Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hisa za Apple zaporomoka marufuku ya iPhone za serikali ya China

Hisa Za Apple Zaporomoka Marufuku Ya IPhone Za Serikali Ya China Hisa za Apple zaporomoka marufuku ya iPhone za serikali ya China

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Hisa za kampuni ya Apple zimeshuka kwa siku ya pili mfululizo baada ya ripoti kuwa wafanyakazi wa serikali ya China wamepigwa marufuku kutumia simu za iPhone.

Thamani ya soko la hisa la kampuni hiyo imeshuka kwa zaidi ya 6%, au karibu dola bilioni 200 (£160bn), katika siku mbili zilizopita.

Uchina ni soko la tatu kwa ukubwa la kampuni hiyo kubwa ya teknolojia, ikichukua 18% ya mapato yake yote mwaka jana.

Pia ndiko ambapo bidhaa nyingi za Apple zinatengenezwa na msambazaji wake mkubwa Foxconn.

Jarida la Wall Street liliripoti Jumatano kwamba Beijing iliwaagiza maafisa wa wakala wa serikali kuu kutoleta simu za iPhone ofisini au kuzitumia kazini.

Siku iliyofuata, Bloomberg News iliripoti kwamba marufuku hiyo inaweza pia kuwekwa kwa wafanyikazi katika kampuni zinazomilikiwa na serikali na mashirika yanayoungwa mkono na serikali.

Ripoti hizo zilikuja kabla ya uzinduzi wa iPhone 15, unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Septemba.

Hakuna taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya China kujibu ripoti hizo.

Apple ina tathmini ya juu zaidi ya soko la hisa duniani, ikiwa ni karibu dola trilioni 2.8.

Chanzo: Bbc