Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hifadhi ya Serengeti, resort Diamond ya Zanzibar zatwaa tuzo ubora Afrika

61437 Hifadhipic

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na resoti ya Diamonds La Gemma dell'Est ya Zanzibar zimetwaa tuzo ya ubora mwaka 2019 zinazotolewa na taasisi ya World Travel Awards inayoandaa tuzo hizo kila mwaka.

Akifafanua kuhusu tuzo hizo zilizotolewa Mauritius hivi karibuni, kamishna msaidizi mwandamizi wa mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete  katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema ni mara ya pili kwa hifadhi ya Serengeti kutwaa tuzi hiyo.

Amesema mwaka 2018 ilishinda kupitia mtandao maarufu wa safari za utalii duniani wa safaribookings.com.

“Washindi katika tuzo za WTA hupigiwa kura na wabobezi katika masuala ya safari na utalii duniani kote. Ushindi wa Serengeti unatokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Tanapa kusimamia hifadhi ikiwa ni pamoja na kuzitangaza ili kuvutia watalii wengi zaidi nchini."

"Tunaishukuru Serikali, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kufanikisha ushindi huu,” amesema Shelutete.

Ameongeza,  “Ukilinganisha na hifadhi nyingine kama Kluger au Masai Mara ya Kenya,  hifadhi zetu bado zina uasilia ule ule uliokuwepo tangu awali. Wenzetu wameshafanya maendelezo mengi yaliyoondoa uasili uliokuwepo."

Pia Soma

Akifafanua tuzo hizo baada ya kuulizwa na Mwananchi,  Shelutete amesema  mikakati iliyopo ni kuendelea kusimamia sheria na kanuni ya uhifadhi na mazingira ya hifadhi hizo.

“Tutaendelea kuongeza wataalamu wa hifadhi ili wasimamie uhifadhi wa mazingira na uasilia wake. Tunajua kuna mahitaji makubwa ya ardhi kwa wananchi wanaotaka kuvamia hifadhi zetu. Tutahakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kwa kuongeza askari wa wanyamapori. Hatutaruhusu waingize mifugo kwenye hifadhi."

Chanzo: mwananchi.co.tz