Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hifadhi ya Serengeti kinara kwa ubora Duniani

Zebras Serengeti Savana Plains Tanzania 660x400 Hifadhi ya Serengeti kinara kwa ubora Duniani

Fri, 5 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Mtandao maarufu wa kurahisisha usafirishaji hasa wa kitalii ujulikanao kama Trip Advisor umetoa orodha ya hifadhi 25 zinazopendwa zaidi duniani zilizoshinda Tuzo za ‘Traveller’s Choice Awards’ huku Tanzania ikiibuka kileleni na pia kuingiza hifadhi tatu katika orodha hiyo.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na mandhari yakuvutia pamoja na wanyama wa aina mbalimbali.

Hifadhi nyingine zilizoshinda tuzo hii kutoka Tanzania, Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12 huku Hifadhi ya Taifa Tarangire yenye kusifika kwa kuwa na Tembo wengi ikishika nafasi ya 14.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika kushinda tuzo hizi huku Kenya ikiwakilishwa na mbuga ya Masai Mara katika nafasi ya tatu na Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini ikishika nafasi ya tano.

MFUNGWA ALIVYOMUACHA HOI MAGUFULI KWA KICHEKO “AKIMUONGELESHA MGOGO KIGOGO”

Chanzo: millardayo.com