Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hekta 20 kwa Zambia Bandari Kavu ya Kwala

Samia Hichilema Zambialeo (600 X 344) Hekta 20 kwa Zambia Bandari Kavu ya Kwala

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa kutambua mchango wa Zambia katika uchumi wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imetenga hekta 20 katika Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya Zambia.

Rais Samia ameyasema hayo akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia leo Oktoba 24, 2023 ambapo yeye ndiye mgeni rasmi.

Zambia ni mteja mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam, ikichukua asilimia 34 ya mizigo yote inayopitia bandari hiyo kwenda nje ya Tanzania.

Aidha, asilimia 80 ya mizigo yote inayopita Bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi, hupita katika mpaka wa Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live