Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hazina yakabidhiwa Sh27 bilioni zilizotaifishwa na Mahakama

60711 PIC+MADINI

Fri, 31 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Kilo 325 ya dhahabu, fedha taslimu Sh305 milioni na magari mawili yaliyotaifishwa na Mahakama baada ya washtakiwa kutiwa hatiani kwa makosa ya rushwa na kusafirisha dhahabu kinyume cha sheria imekabidhiwa Hazina.

Makabidhiano hayo yamefanyika ofisi ndogo za Benki Kuu (BoT) Jijini Mwanza leo  Mei 31, 2019 na kushuhudiwa na viongozi kadhaa wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

Akikabidhi vitu hivyo, Mkurugenzi Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema hatua hiyo imetokana na washtakiwa wanne waliohukumiwa kifungo au faini kutokata rufaa.

“Amri ya Mahakama ya Hakimu mkazi Mwanza ilikuwa ni ya kutaifisha kilo 319 za dhahabu. Kiwango kingine cha kilo  5.8 ilikamatwa mkoani Geita ndio maana nimekabidhi kilo 325 za dhahabu," amesema Mganga

Mizani ya kupimia madini pamoja na mashine ya kupima ubora na thamani ya madini pia imekabidhiwa hazina.

Akipokea vitu hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu  Kazungu amepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kulinda rasilimali za umma kwa faida, maslahi na maendeleo ya Taifa.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz