Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya ndio matumizi sahihi ya gesi majumbani kuepuka mlipuko

72154 Gesipic

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Kama wewe ni mtumiaji wa gesi ya nyumbani na huwa unaisafirisha kutoka dukani hadi nyumbani kwa kutumia bodaboda hii ina kuhusu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji linatahadharisha kuwa ukisafirisha mtungi wa gesi kwa bodaboda ukiwa umeulaza unatakiwa kuachwa kwa dakika 30 hadi dakika 45 kabla ya matumizi kwa sababu unaweza kusababisha mlipuko.

Akizungumza na Mwananchi Kamanda wa kikosi hicho mkoani Mtwara, Christina Sunga amesema hiyo ni kutokana na gesi kubadilisha mwelekeo hasa kama itakuwa imepakiwa katika bodaboda ikiwa imelazwa, badala ya kusimamishwa.

“Unaposafirisha na bodaboda wengi huwa wanalaza mitungi hivyo gesi inabadilisha mwelekeo na nyingi inakuwa imesogea katika eneo la mdomo.”

“Ukiishusha na kuiwasha inaweza kuwa na moto mkali kuliko kawaida au kichwa kinaweza kufyatuka kutokana na kasi yake,” amesema Christina.

Ameongeza, “Ndiyo maana tumekuwa tukitoa elimu kwaa wananchi kupitia redio na televisheni kuhakikisha wanachukua tahadhali juu ya suala.”

Pia Soma

Mmoja wa watumiaji wa gesi, Alice Mpagape amesema hakuwa akifahamu jambo hilo, “Mimi nilidhani ni kwa sababu imejaa ndiyo maana inawaka kwa nguvu kumbe ni tatizo.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz