Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatua kwa hatua sakata la makontena ya Makonda

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kitendo cha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kumshukia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu sakata la mnada wa makontena 20 yaliyopo bandarini ni kama kimerejesha upya sakata hilo lililoanza tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Makontena hayo yenye samani za kama viti, meza na mbao za kuandikia yenye umiliki wa Paul Makonda yanadaiwa kodi inayokadiriwa kuwa Sh1.2bilioni.

Jumamosi iliyopita Agosti 25, 2018 makontena hayo yalikosa wanunuzi katika mnada kutokana na watu wengi kushindwa kufikia bei iliyotajwa.

Soma Zaidi:

Makontena ya Makonda yakosa wateja

Baada ya makontena hayo kutouzika, Jumapili Agosti 26, 2018 Makonda alitoa onyo kuwa mtu atakayenunua makontena hayo atalaaniwa yeye (mnunuzi) na uzao wake.

Akikagua makontena hayo Agosti 27, 2018, Waziri Mpango aliwataka viongozi serikalini kuchunguza maneno yao na akawaomba wanaotaka kununua samani hizo wasiogope.

Februari 2018

Makonda aliwapeleka baadhi ya walimu wa jijini Dar es Salaam, waandishi wa habari na wadau wengine kwenda bandarini kuwaonyesha makontena yenye vifaa vya ofisi na vya kufundisha, akisema vimetolewa na Watanzania waishio Marekani.

Hata hivyo, vifaa hivyo vilionekana ndani ya makontena vikiwa vimeshaunganishwa, tofauti na hali ya kawaida ya kusafirisha bidhaa zikiwa hazijaunganishwa ili kuziweka nyingi kwenye kontena moja kwa ajili ya nafasi.

Mei 10, 2018

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo aliieleza MCL Digital kuwa mamlaka hiyo imetoa notisi ya siku 30 kwa waagizaji wa mizigo ambayo imekaa bandarini kwa zaidi ya siku 90 kuchukua mizigo yao na kulipa stahiki zinazotakiwa.

Soma Zaidi:

TRA yatishia kuuza mali za Makonda

Mei 12, 2018

Kaimu Kamishna wa Ushuru na Forodha wa TRA, Ben Asubisye alisema wamiliki wa mizigo hiyo wanatakiwa kuikomboa ndani ya siku 30 kuanzia siku hiyo.

Katika tangazo hilo lililokuwa na orodha ya makontena zaidi ya 800, jina la Paul Makonda lilijitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20 yakiwa na bidhaa kadhaa zikiwemo za samani.

Mei 18, 2018

Wakati utata ukiendelea juu ya umiliki wa makontena 20 yaliyotajwa na TRA kuwa miongoni mwa yale yatakayopigwa mnada kwa kukaa bandarini muda mrefu, Makonda alisema hajui chochote na amesikia habari hizo kwenye magazeti kama walivyozisikia watu wengine.

Makonda alitoa kauli hiyo wakati akizindua kamati ya mapendekezo kuhusu wanawake waliotelekewa na wenza wao.

Sidhani kama nahusika na jambo lolote lile na sijui chochote, hilo unalolisema hata mimi nimesoma kwenye magazeti kama ulivyosoma wewe. Nafikiri zilikuwa ni habari za jana na leo nimesoma nyingine,” amesema.

Makonda ayakana makontena ya Paul Makonda bandarini

Mei 20, 2018

Barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilieleza kuwa mali zilizomo ndani ya makontena 20, ambayo ni mali ya mtu anayeitwa Paul Makonda zina thamani ya Sh1.4 bilioni, ikieleza kuwepo kwa ombi la msamaha wa kodi wa mali hizo, maombi ambayo hayastahili kuridhiwa, kwa mujibu wa Sheria ya Kodi.

Kadhalika barua hiyo ambayo si TRA wala Dk Mpango waliothibitisha kuitambua, imeandikwa na mamlaka hiyo ya ukusanyaji kodi kumueleza waziri husika kuwa ombi hilo haliwezekani kwa kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa haina sifa ya kupata msamaha kwa mujibu wa sheria.

Barua hiyo ilitaja kiwango hicho cha samani ya mali hizo, ikirejea ombi la msamaha wa kodi lililowasilishwa na ofisi hiyo ya mkoa.

Soma zaidi

Msimamo wa Dk Mpango dhidi ya Makonda mjadala

TRA yatishia kuuza mali za Makonda

Chanzo: mwananchi.co.tz