Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatua 4 zilizochukuliwa na Benki Kuu Tanzania kudhibiti athari za COVID-19

38244 BOT+PIC UVIKO -19 Kuwatenga Vijana na huduma za fedha.

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni Agosti 12, 2021 Benki Kuu ya Tanzania na AfPI, taasisi inayoongoza duniani kwenye sera na kanuni za huduma jumuishi za fedha, kwa pamoja zimefanya mkutano kwa ajili ya viongozi wa taasisi za usimamizi wa sekta ya fedha barani Afrika ili kutafuta utatuzi kwa makundi yaliyo kwenye hatari ya kutengwa kutokana na janga la UVIKO-19.

BOT na AFI na muungano wa uongozi wa sera za huduma jumuishi za fedha duniani wamekutana kimtandao kwa lengo la kujadili, kubadilishana uzoefu na kutafuta suluhu za kibunifu ili kukwamua makundi yaliyo katika hatari ya kutengwa.

Prof. Florens Luoga ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. "Utendaji kazi wetu wa muda mrefu pamoja na AFI umejengwa katika pande mbili, ambazo ni ushirikiano wa kisera na usaidizi wa kitaalamu katika kuhakikisha hatuyaachi nyuma makundi ambayo yanaathirika zaidi katika majanga, mfano katika janga la UVIKO-19,” amesema

“Hivyo, tunafurahi kufanya kazi pamoja na AFI kwa miaka miwili mfululizo katika kuhakikisha wajumbe wa AfPI tunakutana, na kushiriki kwa kutoa uzoefu wetu na kujifunza toka kwa wenzetu,” - Gavana Prof. Luoga.

Hatua 4 zilizochukuliwa taasisi hizo ni pamoja:

1. Kulegeza sera za fedha na kuzihamasisha benki kuahirisha ulipaji wa mikopo. 2. Kupunguza riba na kuongeza muda kulipa mikopo ili kutoa unafuu wa kifedha kwa wateja. 3. Kukuza mifumo ya malipo kidigitali kufuatia kuanzishwa kwa mfumo wa muingiliano (interoperability) katika malipo. 4. Kuanzishwa kwa mfumo wa kusajili watoa huduma za fedha.

Katika kikao hicho, Gavana Profesa Luoga ameungana na magavana na manaibu gavana kutoka Burundi, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Namibia, Rwanda, Senegal, Seychelles, Sierra Leone na Zimbabwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live