Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hasunga aeleza faida za tumbaku nchini, asema hawezi kuzuia matumizi yake

86596 Tumbakupic Hasunga aeleza faida za tumbaku nchini, asema hawezi kuzuia matumizi yake

Sun, 1 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga amesema hayupo tayari kupiga marufuku matumizi ya tumbaku nchini licha ya kuwa na madhara kiafya kwa sababu zao hilo ni la pili kwa kuingiza fedha za kigeni.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 30, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari, kubainisha kuwa kampeni za kupinga matumizi ya tumbaku ni moja ya changamoto ya ukuaji wa zao hilo.

“Tunajua kuna changamoto nyingi sasa hivi kuna watu wengi wanapiga kampeni ya kupinga matumizi ya tumbaku, wanasema ina madhara, lakini sisi tunaamini hata kama ina madhara tunasema kila mtu anaruhusiwa kuvuta sigara lakini ina madhara kwa afya,” amesema Waziri Hasunga. 

Amesema kwa kuwa tumbaku ina madhara kiafya watu wako huru kuamua kuvuta au kutovuta.

“Unavuta kidogo ili ujisikie furaha yako kiasi. Hizi kampeni za kupinga uvutaji wa tumbaku, mimi kama waziri nadhani siko tayari kupiga marufuku. Hili ni zao la pili kwa Tanzania kwa kuingiza fedha za kigeni,” amesema Hasunga.

“Ikitoka korosho inaingia tumbaku. Sasa ukipiga marufuku halafu tufanye nini? Hizi hela ndiyo tutawekeza pengine. Baadaye sasa tukiwa na hela ya kutosha tutaangalia, je tuendelee au tusiendelee,” amesisitiza.

Hata hivyo alisema hahamasishi Watanzania kuendelea kuvuta sigara, bali lengo kupata soko la nje.

“Sisi kwetu Tanzania uvutaji siyo mkubwa sana na mimi nawahimiza Watanzania wasiendelee kuvuta sana, lakini wale wanaovuta nchi za nje tupate hela,” amesema.

Awali Waziri Hasunga amesema katika msimu uliopita kulikuwa na lengo la kuzalisha kilo 57.30 milioni, kwamba tumbaku iliyonunuliwa mpaka mwisho wa msimu ni zaidi ya kilo 60.69 milioni zenye thamani ya zaidi ya Dola 92.92 milioni sawa na asilimia 105.9 ya lengo.

Chanzo: mwananchi.co.tz