Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hasunga: Mkapa alitilia mkazo kilimo chenye tija 

E9c14569e32b6650efa4091f4e0e16cd Hasunga: Mkapa alitilia mkazo kilimo chenye tija

Tue, 28 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema wakulima na wizara yake imempoteza Benjamin Mkapa kama kiongozi ambaye si tu kwamba alisisitiza Watanzania kutumia nguvu zao kama mtaji katika kufanya kazi bali aliyehakikisha kilimo kinatoa mchango mkubwa katika maendeleo yao na taifa.

Waziri Hasunga alisema kuna mambo mengi ambayo tunajivunia leo kwenye kilimo ambao yametokana na mchango mkubwa wa Mkapa.

Hasunga aliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni msimamo wake thabiti katika kuhakikisha wataalamu wa kilimo kwa ngazi zote wanatoka maofisini na kwenda kutoa ushauri kwa wakulima na wafugaji ili kilimo kinachotegemewa na zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania kitoe mchango unaostahili.

“Aliposema mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, alisisitiza watu kutumia nguvu zao kama mtaji katika uzalishaji mali kwa kufanya kazi mbalimbali hasa za kilimo ili kutokomeza njaa na umasikini kwenye kaya,” alisema.

Pia alitaja uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) ilikuwa ni moja ya jitihada za kusaidia kaya masikini ambazo nyingi zipo vijijini zinajishughulisha na kilimo.

Katika kukabiliana na rushwa aliziasha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na (Takukuru) ili masikini wapate haki kwenye ofisi za serikali na kwenye maeneo mengine wanapokwenda kutafuta huduma.

Chanzo: habarileo.co.tz