Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halotel yazindua laini za VIP zenye gharama nafuu

8836 Halotel+pic TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya Halotel imezindua laini za watu mashuhuri zitakazo wawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu zaidi kwa kila dakika na MB za intaneti watakazotumia.

Laini hizo zitawawezesha wateja kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno au kutumia intaneti bila ulazima wa kujiunga na kifurushi chochote.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda alisema laini hizo ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wao watakaoweza kutumia simu bila hofu.

“Huduma hii inawalenga wateja wote, wenye kipato cha chini, kati na juu. Wateja wenye matumizi madogo watapewa laini za silver (fedha) na wenye matumizi ya kati watapewa gold (dhahabu) na diamond (almasi) itatolewa kwa wenye matumizi makubwa,” alisema Semwenda.

Alifafanua kuwa mteja atakayenunua laini za silver inayouzwa Sh5,000 anaweza kupiga simu ndani ya mtandao kwa Sh30 tu kwa dakika wakati gharama za kawaida ni Sh228 ambayo ni sawa na punguzo la mara saba.

Kwenda mitandao mingine, alisema mteja atatozwa Sh45 kwa dakika tofauti na Sh228 za kawada. Kila MB moja mteja atatumia intaneti kwa shilingi nne tu akiwa na laini hiyo tofauti na Sh30.72 zinazotozwa kwa laini ya kawaida huku akifurahia Facebook ya bure.

Chanzo: mwananchi.co.tz