Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri zatakiwa kutenga maeneo ya uwekezaji

Ardhi Pic Mabula Halmashauri zatakiwa kutenga maeneo ya uwekezaji

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, amezitaka halmashauri nchini kutenga maeneo ya uwekezaji, ili kurahisisha wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali bila usumbufu.

Dk Mabula ametoa kauli hiyo Februari 22, 2023 wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika mkoani humo.

Waziri Mabula amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kwa kukaribisha wawekezaji, ambapo alieleza kuwa tayari wawekezaji wameanza kuja kwa wingi na kushindana kwenye sekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda , madini na ujenzi wa nyumba.

Kwa mujibu wa Dk Mabula, Rais Samia alielekeza kila halmashauri nchini kutenga maeneo ya uwekezaji, hivyo ni jukumu la kila halmashauri kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanaandaliwa na kutengwa sambamba na kuwekewa mkakati utakaofanya maeneo hayo kuwa tayari kwa uwekezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live