Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri Kinondoni, Ubungo zatakiwa kuwasilisha mapato TRA

Fedhapic Halmashauri Kinondoni, Ubungo zatakiwa kuwasilisha mapato TRA

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni wamebaini Halmashauri za Kinondoni na Ubungo hazijawasilisha mapato ya kodi ya zuio kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hayo yamesemwa leo Jumanne Novemba 7, 2023 na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Elizabeth Mokiwa amesema walifanya uchambuzi wa mfumo kuhusu ukataji na uwasilishaji wa kodi ya zuio katika ununuzi wa vifaa na huduma.

Amesema lengo la uchambuzi huo ni kuboresha na kuimarisha matumizi ya risiti za mashine za EFD na ukataji wa kodi ya zuio.

Mokiwa amesema uchambuzi umebaini mwaka wa fedha 2022/23 Manispaa ya Kinondoni ilikata kodi ya zuio kwa bidhaa na huduma ambapo Sh89.4 milioni bado hazijawasilishwa TRA na mwaka wa fedha wa 2021/22 na 2022/23 Sh53.8 milioni hazijawasilishwa na kwa Manispaa ya Ubungo.

"Tumewashauri Wakurugenzi wa Manispaa hizo kuhakikisha fedha zote zinawasilishwa kwa TRA," amesema Mokiwa.

Mokiwa amesema wamefuatilia miradi 11 ambayo ni ujenzi wa shule, ujenzi wa soko, maboresho ya vibanda vya biashara na uchimbaji wa mfumo wa maji taka.

Amesema Sh1.522 bilioni ni mradi wa ujenzi wa shule mbili mpya za msingi za Kunduchi, Mapinduzi pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa ya msingi na awali kwa shule za msingi tano.

Shule ambazo zinajengwa kupitia mradi wa Boost ni Ali Hassan Mwinyi, Kisauke, Mtambani, Mkwawa na Mchangani mradi umekamilika lakini kwa shule ya Msingi Mapinduzi ujenzi ulichelewa baada ya mabadiliko ya michoro.

Amesema kuna miradi imechelewa kutokana na changamoto mbalimbali huku mingine ikiendelea kwa kuwa ndani ya muda wa uendelezaji wa ujenzi.

"Uchelewaji wa ujenzi wa shule ya Mapinduzi ni kutokana na ufinyu wa eneo la mradi na kusababisha mabadiliko ya michoro kutoka madarsa msambao na kuwa ghorofa," amesema.

Amesema wakati ujenzi wa Shule ya Msakuzi Kusini wenye thamani ya Sh475 milioni unaendelea kwa kuwa bado upo ndani ya muda watahakikisha unakamikika kwa wakati na kwa ubora.

Mokiwa amesema wanafuatilia ujenzi wa Soko la Mivumoni lililoanza kujengwa tangu 2020 lenye thamani Sh152 milioni ili limalizike na wananchi wa maeneo hayo na majirani waweze kulitumia soko hilo.

Pia Mokiwa amesema wamefuatilia Sh100 milioni za mradi wa maboresho ya vibanda vya soko la Simu 2000 ambapo kumekuwa na mapungufu katika uwekaji gata na sehemu ya maegesho ya magari.

Amesema uwepo wa changamoto za mindombinu zimechangia uchelewaji wa mradi wa uchimbaji wa mfumo wa maji taka wenye thamani ya Sh1.4 bilioni ambao unakutana na miundombinu ya maji safi na umeme ambapo mradi ulitakiwa kukamilika mwezi Septemba 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live