Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ya hewa yasababisha ndege za ATCL, Precision kushindwa kutua uwanja wa Dodoma asubuhi

98053 Ndege2+pic Hali ya hewa yasababisha ndege za ATCL, Precision kushindwa kutua uwanja wa Dodoma asubuhi

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Abiria waliokuwa wakisafiri kwa kutumumia ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na Kampuni ya Precision walikwama kwa saa mbili na kulazimika kurejea Dar es salaam kutokana na hali ya hewa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Ndege hizo zilizokuwa zitue katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kati ya saa moja na saa mbili zilishindwa  kutokana na hali ya hewa iliyokuwa uwanjani hapo. Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Machi 5,2020 meneja masoko na uhusiano wa kampuni ya Precision, Hillary Mremi amesema ndege aina ya PW600 ikiwa na abiria 39 iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12 asubuhi lakini ililazimu kurejea kabla ya kutua baada ya rubani kukuta hali mbaya ya hewa pamoja na ukungu. "Baada ya rubani kufika katika anga la Dodoma akiwa anajiandaa kutua alikutana na hali mbaya ya hewa pamoja na ukungu na kumlazimu kuirudisha ndege Dar es Salaam,"amesema Mremi.

Amesema alipata taarifa hali ya hewa imesharejea kawaida wakati akijiandaa kutua na kumlazimu kuongeza mafuta kabla ya kuanza safaria saa 3:15 na kutua Dododma saa 4:40," amesema. Hata hivyo, Mremi aliongeza kuwa ndege aina ya PW601 ikiwa na abiria 52 ilifanikiwa kuondoka katika Uwanja wa Dodoma na kutua Dar es Salaam baada ya kushindwa kuondoka kwa muda uliopangwa. Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi amesema wakati wa asubuhi kuna baadhi ya maeneo yanakuwa na ukungu kutokana na hali ya hewa ikiwemo Dodoma. "Majira ya asubuhi kulikuwa na ukungu baada ya kubaini hilo ilimlazimu rubani kurudi Dar es Salaam kwa muda hata hivyo ndege imeshaondoka na hakuna abiria aliekwama," amesema Matindi Amesema kuna baadhi ya viwanja vya ndenge ambavyo rubani ana uwezo wa kutua moja kwa moja na vingine ili kutua ni lazima aone moja kwa moja ikiwemo cha Dodoma.

Chanzo: mwananchi.co.tz