Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hadi 2025 wananchi watakuwa na uelewa wa masuala ya fedha - Serikali

Hadi 2025 Wananchi Watakuwa Na Uelewa Wa Masuala Ya Fedha   Serikali.jpeg Hadi 2025 wananchi watakuwa na uelewa wa masuala ya fedha - Serikali

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inakusudia ifikapo mwaka 2025 takriban asilimia 80 ya wananchi watakuwa wamepata uelewa wa masuala ya fedha.

Hayo yamebainishwa na leo Jijini Dodoma na Kamishna wa Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya fedha Dkt. Charles Mwamwaja wakati akizungumza na wanahabari kueleza maadhimisho ya wiki za fedha Kitaifa yatakayoanza tarehe 20-26 mwaka huu jijini Arusha.

Amesema kutokana na utafiti wa FinScope wa mwaka 2023 nchin, ni asilimia 53 8 tu ya nguvu kazi wanatumia Huduma rasmi za fedha na hivyo kubaki na kundi kubwa la watanzania ambao hawafaidiki na huduma hizo na hivyo kukosa fursa za kuboresha maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zingewezesha kuchangia katika pato la Taifa.

"Maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha ni utekelezaji wa mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha wa mwaka 2020/2021-2029-2030"

Elimu Kwa Umma ni pamoja na maeneo ya kipaumbele Katika utekelezaji wa mpango huo.

Aidha, Dkt Mwamwaja amesema katika hatua ya utekelezaji huo Wizara ya fedha imeandaa program ya kutoa elimu kwa Umma ya mwaka 2021/22-25/26 na programu hiyo imeweka mikakati ikiwa ni pamoja na matukio na mbinu mbalimbali zitakazotumika katika utoaji wa elimu ya fedha kwa Umma.

Hata hivyo wiki ya huduma za fedha inalenga kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo: watumishi wa Umma, wanafunzi, wakufunzi, watu wenye mahitaji maalumu, wajasiriamali wadogo na wa kati, asasi za kiraia, wahariri na waandishi wa vyombo vya habari watoa huduma za fedha, watoto na Umma Kwa ujumla.

Kauli mbinu ya maadhimisho hayo ni "Elimu ya fedha, msingi wa maendeleo ya kiuchumi"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live