Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima awauma sikio wanawake wajasiriamali

Waziri Gwajima Alaani Mauaji Ya Mzee Minza Madaha Gwajima awauma sikio wanawake wajasiriamali

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsi na Makundi Maalum,Dk Dorothy Gwajima amewataka wanawake wajasirimali nchini kutumia mitandao ya kijamii kwaaajili ya kutangaza bidhaa wanazozalisha ili kupata masoko ndani na nje ya nchi.

Dk Gwajima ameyasema hayo wakati wa kukagua mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na wanawake mbalimbali kwaajili ya maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini yaliyofanyika Kijiji cha Olevolos, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha yenye kauli mbiu isemayo "Wezesha Wanawake Wanaoishi Kijijni Kwa Uhakika wa Chakula ,Lishe na Uendelevu wa Familia"

Amesema endapo watafungua akaunti kupitia mitandao ya kijamii wataweza kupata masoko kwaajili ya kuuza bidhaa zao wanazozalisha zinazotokana na ubunifu wanaofanya na kuunganishwa na masoko ndani ya nchi na nje.

Amesisitiza wanawake kuendelea kuzalisha zaidi chakula ili kuhakikisha lishe zinapatikana ndani ya familia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live