Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gmail zisizotumika muda mrefu kufutwa

Gmail Kufutwa.png Gmail zisizotumika muda mrefu kufutwa

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ama hujawahi kuitumia akaunti yako ya Gmail kwa miaka miwili, jiandae kuipoteza ijumaa hii Desemba 1, 2023 kwani kampuni ya Google ambayo ndio mmiliki wa ‘aplikesheni’ hiyo itazifuta kama njia moja wapo ya kupambana na utapeli wa mitandaoni.

Kampuni hiyo ilisema itawatumia watumiaji taarifa kadhaa kwamba akaunti zao za Gmail zinatarajiwa kufutwa, hivyo kuwapa muda wa kuingia na kuyachukua maudhui pamoja na taarifa muhimu wanazozihitaji bado.

Hatua hii inakuja miezi sita tangu, Google itangaze mabadiliko ya sera zake kwa ajili ya kulinda watuaji wa mitandao yao.

Sera mpya ya Google iliyobadilishwa inasema: “Ikiwa akaunti haijatumika kwa muda mrefu, kuna uwezekano mkubwa wa kuathirika. Hii ni kwa sababu akaunti zilizosahauliwa au zisizotunzwa mara nyingi hutegemea manenosiri ya zamani au yaliyotumika tena ambayo huenda yameingiliwa, hayajaweka uthibitishaji wa vipengele viwili, na hupokea ukaguzi mdogo wa usalama na mtumiaji,”

Takwimu za Google zinaonyesha kwa mwezi mmoja zaidi ya watu bilioni 1.8 hutumia Gmail.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live