Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gharama zilizidi bajeti Uwanja wa Ndege Chato

Chato Chato Uwanjaaa Gharama zilizidi bajeti Uwanja wa Ndege Chato

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema gharama za ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita zilizidi bajeti iliyotengwa kwa sababu ulifanyika bila upembuzi yakinifu.

Kutofanyika kwa upembuzi huo, amesema kunaongeza hatari kwa Serikali kuwekeza katika mradi usio na tija na uwezekano wa kuwapo gharama zisizodhibitiwa na ongezeko la muda katika utekelezaji wake.

“Mapitio yangu yalibaini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) hawakufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kwa ujenzi,” amesema Kichere.

Kichere amesema Sh3.62 bilioni za mradi huo zilitolewa kwenye miradi mingine kwa matarajio kwamba zingerejeshwa baada ya Hazina kutoa fedha zake, jambo ambalo halikutekelezwa kwa wakati hivyo kusimamisha miradi mingine iliyopangwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live