Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gharama za maisha Afrika Mashariki zatajwa kuwa Juu

Mfumuko Wa Bei Zimbabwe Gharama za maisha Afrika Mashariki zatajwa kuwa Juu

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia imepunguza kiwango chake cha makadirio ya ukuaji wa uchumi, huku ikitahadharisha kuwa baadhi ya nchi zinakabiliwa na mporomoko wa uchumi kwasababu ya vita ya Urusi nchini Ukraine bna virusi vya corona.

Imeeleza kuwa ipo hatari kubwa kudolola kwa ukuaji wa uchumi, na ukosefu wa ajira huku mfumuko wa bei ukiongezeka – na hali hii inaweza kurejea kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1970, iliyosababisha kupanda kwa bei za vyakula na mafuta.

Mkuu wa Benki hiyo, David Malpass, alisema ni vigumu kutazama upande mwingine wa mzozo.

Alisema kuwa baadhi ya nchi zinazoendelea zinakabiliwa na deni kubwa, huku serikali zikishindwa kununua bidhaa.

Kiwango cha makadirio ya ukuaji mpya wa uchumi wa dunia cha benki hiyo kwa sasa ni cha -2.9% - kiwango hiki kikionyesha kuporomoka kwa uchumi wa dunia ambako hakujawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 80.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live