Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gharama za intaneti pasua kichwa nchi zinazoendelea

Intanentiiiiiii Gharama za intaneti pasua kichwa nchi zinazoendelea

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuongezeka kwa idadi ya Watumiaji wa Intaneti Duniani ambao ni takriban Bilioni 5, inaelezwa kuwa bado gharama za manunuzi ya huduma hiyo ni pasua kichwa.

Ripoti mpya ya Shirika la Muungano wa Mawasiliano Duniani (ITU) inasema Watu Bilioni 2.9 bado hawatumii kabisa Mitandao, na Mamilioni wanakumbwa na changamoto ya gharama na ubora wa Intaneti wa hali ya chini

Ripoti hiyo inasema gharama ya Huduma za Mitandao na vifaa vya kidigitali bado ni changamoto. Inaelezwa kuwa, gharama kwa Nchi zenye Uchumi wa Chini na Kati ni kubwa ikilinganishwa na Mataifa yaliyoendelea

Chanzo: www.tanzaniaweb.live