Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghana yazindua mtambo mkubwa wa sola

Umeme Jua Solar.png Ghana yazindua mtambo mkubwa wa sola

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ghana imezindua mtambo wa kufua umeme wa jua wenye uwezo wa volt 16.82 megawatt katika paa moja kubwa huko Tema, mradi unaotajwa kuwa mkubwa zaidi barani Afrika.

Mradi huo wenye thamani ya dola milioni 17 unamilikiwa na LMI Holding Company Limited, na unatarajiwa kusambaza umeme wa jua kwa wateja ndani ya eneo la viwanda la Tema Free Zone Enclave (TFZE).

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti Jumatatu Julai 29 kuwa mradi huo ambao pia unajulikana kama Mradi wa Mega Warehouse Rooftop Solar PV, unachukua kilomita 95,745 (sawa na viwanja 20 vya mpira wa miguu) na unatarajiwa kuzalisha GWh 24.7 za nishati safi kila mwaka.

“Mradi huu ulifadhiliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) na uko tayari kuchukua jukumu muhimu katika kuendeleza nishati mbadala ndani ya mazingira ya viwanda ya Ghana,” taarifa ya LMI Holding ilisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live