Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gesi asilia kuwafikia Watanzania wote

Gesiii Gesi asilia kuwafikia Watanzania wote

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Biteko amesema kuwa, Mkakati wa Wizara ya Nishati ni kuhakikisha kuwa inasimamia ipasavyo Sera ya Nishati ya mwaka 2015 na kuhakikisha kuwa kunakuwa na upatikanaji wa nishati safi ambayo itawafikia wateja mbalimbali kwa urahisi na bei nafuu. - Amesema kuwa, lengo la nchi ni kuwa na nishati inayotokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo Jua, Upepo, Gesi na Maji ili Gesi Asilia iliyopo itumike pia kwa kiasi kikubwa kwenye maeneo mengine kama viwanda na majumbani badala ya kutumika kwa kiasi kikubwa kwenye umeme na pia kupunguza matumizi ya mafuta. - Dk Biteko ameeleza mikakati hiyo leo Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi katika hafla ya utiaji saini ya mkataba wa mauziano ya gesi asilia itakayozalishwa eneo la Ntorya, kitalu cha Ruvuma, kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kampuni ya ARA Petroleum ya Oman na Ndovu Resources ya Uingereza. - Ameeleza kuwa, katika kitalu cha Ruvuma, gesi iliyogunduliwa na kuhakikiwa ni futi za ujazo bilioni 1.6. Mradi uliosainiwa utakuwa wa kwanza kufanyika nchini na utawezesha kupunguza kiu ya watanzania kutumia gesi asilia hata kwa maeneo yaliyo mbali na miundombinu ya mabomba na hivyo kuchochea matumizi ya nishati safi nchini.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Biteko amesema kuwa, Mkakati wa Wizara ya Nishati ni kuhakikisha kuwa inasimamia ipasavyo Sera ya Nishati ya mwaka 2015 na kuhakikisha kuwa kunakuwa na upatikanaji wa nishati safi ambayo itawafikia wateja mbalimbali kwa urahisi na bei nafuu. - Amesema kuwa, lengo la nchi ni kuwa na nishati inayotokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo Jua, Upepo, Gesi na Maji ili Gesi Asilia iliyopo itumike pia kwa kiasi kikubwa kwenye maeneo mengine kama viwanda na majumbani badala ya kutumika kwa kiasi kikubwa kwenye umeme na pia kupunguza matumizi ya mafuta. - Dk Biteko ameeleza mikakati hiyo leo Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi katika hafla ya utiaji saini ya mkataba wa mauziano ya gesi asilia itakayozalishwa eneo la Ntorya, kitalu cha Ruvuma, kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kampuni ya ARA Petroleum ya Oman na Ndovu Resources ya Uingereza. - Ameeleza kuwa, katika kitalu cha Ruvuma, gesi iliyogunduliwa na kuhakikiwa ni futi za ujazo bilioni 1.6. Mradi uliosainiwa utakuwa wa kwanza kufanyika nchini na utawezesha kupunguza kiu ya watanzania kutumia gesi asilia hata kwa maeneo yaliyo mbali na miundombinu ya mabomba na hivyo kuchochea matumizi ya nishati safi nchini. Makubaliano hayo pia yamehusisha kuanzisha mahusiano ya kujenga miundombinu ya gesi asilia imesainiwa kati ya TPDC na Kampuni ya KS Energy, pia kuanzisha mahusiano ya kujenga miundombinu ya kusambaza Gesi Asilia kwa teknolojia ya miundombinu midogo ya kubadilisha Gesi Asilia kuwa kimiminika (Mini-LNG). - “Mkakati wetu ni kubadilisha suala hili la Gesi Asilia kutumika zaidi kwenye umeme ambayo ni takriban asilimia 80, tunataka kuwe na nishati mchanganyiko nchini ili gesi itumike kwenye viwanda na majumbani na pia tupunguze utegemezi wa mafuta.” Amesema Dk Biteko -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live