Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana wa BoT: Tuko tayari kununua dhahabu

37887 Pic+gavana Gavana wa BoT: Tuko tayari kununua dhahabu

Wed, 23 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema wako tayari kununua dhahabu moja kwa moja kutoka kwa wachimbaji kwa sababu tangu zamani walikuwa wanafanya hivyo.

Profesa Luoga ameyasema hayo leo wakati wakitoa changamoto na maoni yao katika mkutano wa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini jijini Dar es Salaam.

Amesema kilichotokea waliuziwa dhahabu feki jambo ambalo lilisababisha kusimamisha mchakato huo.

Amesema kufanya hivyo ni moja ya utunzaji wa fedha ukiachana na ile ya utunzaji wa dola za Marekani.

“Tuko tayari kununua dhahabu ambayo tayari iko ‘refined’ (chakatwa) kwa sababu ndiyo kiwango ambacho kinakubalika kimataifa na nimefurahi kusikia kuwa kuna watu wana mitambo ya kufanya hivyo,” amesema.

Amesema kinachofanyika hivi sasa ni majadiliano kati ya BoT, wizara ya madini na tume ya madini katika uanzishwaji wa kituo cha kuuzia dhahabu ili kuondoa kilio cha kukosekana soko.

“Benki kuu tumeandaa sehemu ya kuhifadhi madini ndani ya utaratibu maalumu ambazo tutakubaliana kuwa ni lazima dhahabu inayokuwa pale iwe na mpangilio wake wa uhifadhiwaji.”

“Kwa mfano mnunuzi hajapatikana hiyo dhahabu hairuhusiwi kukaa hapo zaidi ya siku tano na badala yake ipelekwe Center’.”



Chanzo: mwananchi.co.tz