Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana wa Benki Kuu ashinda tuzo ya kimataifa

Gavana 4 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga ambaye pia ni kiongozi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Huduma Jumuishi za Kifedha (AFI), ametunukiwa tuzo “Central Banker of the Year” ya 2021”, inayotolewa na The Banker Magazine, kampuni tanzu ya Gazeti la Financial Times, kutokana na jitihada zake za kuimarisha uchumi katikati ya janga la UVIKO-19.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga ambaye pia ni kiongozi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Huduma Jumuishi za Kifedha (AFI), ametunukiwa tuzo “Central Banker of the Year” ya 2021”, inayotolewa na The Banker Magazine, kampuni tanzu ya Gazeti la Financial Times, kutokana na jitihada zake za kuimarisha uchumi katikati ya janga la UVIKO-19. Gavana Luoga, ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi ya Mipango ya Kisera ya Huduma Jumuishi za Kifedha Kanda ya Afrika (AfPI) ameshinda tuzo hiyo kutokana na jitihada zake za kupiga vita utolewaji wa mikopo kiholela na mpango aliyotangaza mwezi Novemba, mwaka jana kuangalia uwezekano wa kuwa na fedha ya kidijitali inyotolewa na Benki Kuu (Central Bank Digital Currency - CBDC).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live