Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana asisitiza ubunifu Sekta ya Benki

Emmanuel Tutuba Gavana asisitiza ubunifu Sekta ya Benki

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba, amewataka watalaam katika sekta ya Benki nchini kuwa wabunifu ili kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi na kuisadia Serikali kukuza uchumi .

Akizungumza na TBC mara baada ya kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi ya Benki inayotolewa na Taasisi ya Benki Tanzania (TIOB), amesema wataalam wa masuala ya Benki wanapaswa kutumia taaluma zao katika kuongeza ubunifu ili kuwahudumia wananchi.

Gavana Tutuba amesema wataalam wa masuala ya Benki wamesaidia kupunguza changamoto nyingi katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha mikopo umiza kutoka asilimia 11 mwaka 2016 mpaka asilimia 5 mwaka 2023.

Tutuba ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutumia huduma za kibenki kutokana na miongozo na usimamizi imara uliowekwa na BOT kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live