Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GST yarusha 'drone' utafiti wa miamba

Drone Training Banner Commercial GST yarusha 'drone' utafiti wa miamba

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza majaribio ya Utafiti wa Jiosayansi kwa kutumia njia ya kwa kurusha Ndege Nyuki (Drone) kwa kushirikiana na Kampuni ya Ellygreentech katika Kijiji cha Mzogole kilichopo Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

GST imeanza kufanya majaribio ya kurusha Ndege Nyuki kwa ajili ya tafiti za rasilimali zilizopo chini ya ardhi ikiwemo Madini na Maji ili kubaini taarifa sahihi za rasilimali hizo.

Akizungumza na HabariLeo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema vision 2030 itafikiwa kwa kuwa taarifa sahihi za kijiolojia ya miamba ndiyo imebeba dhana ya utajiri wa Tanzania ambapo GST kwa kushirikiana na taasisi nyingine itengeneze kanzidata ya taarifa sahihi za kijiolojia

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Kanzidata ya Taifa ya Rasilimali Madini, Hafsa Maulid amesema GST imejipanga kikamilifu kutekeleza kwa vitendo dhana ya Vision 2030 kwa kufanya tafiti za kina kwa njia ya Jiofizikia angalau asilimia 50 ifikapo 2030 kwa sasa ni asilimia 16 pekee ambayo imefanyiwa utafiti huo.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ellygreentech Elbariki Nsenuka amesema Kampuni anayoiongoza inatumia teknolojia ya kisasa ya kutafiti madini kwa kurusha Ndege Nyuki ambapo Kampuni hiyo ni ya kitanzania na ina wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika tasnia hiyo.

Amesema faida za kutumia Ndege Nyuki ni pamoja na kuokoa muda pamoja na kupata taarifa sahihi na zenye uhakika huku akitoa wito kwa wadau wa Sekta ya Madini na Taasisi zinazohusika na tafiti za miamba na udongo kutumia teknolojia hiyo. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live