Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GGM yatoa bil.9.2/- kwa jamii

Eb6d219f19bd5027053f367dbc9db364 GGM yatoa bil.9.2/- kwa jamii

Wed, 23 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita (GGM) inatoa Sh bilioni 9.2 kila mwaka kama sehemu ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii kupitia Halmashauri ya Mji Geita na Wilaya ya Geita.

Huu ni mwaka wa tatu tangu fedha hizo zianze kutolewa na kutumika kwa shughuli mbalimbali za kijamii ukiwemo ujenzi wa madarasa, viwanda, soko la madini na miradi mingine ya kijamii.

Hayo yamebainishwa na Makamu Rais Miradi Endelevu wa GGM, Simon Shayo, alipozungumza na gazeti hili jana mkoani Geita.

Alisema GGM itaendelea kuwa mdau muhimu kwa maendeleo ya nchi na kinara wa uchimbaji wa dhahabu nchini kutokana na kuwa na wafanyakazi wenye weledi na wanaojituma huku wakilenga maendeleo ya jamii.

“Tunaposherehekea miaka 20 tangu kuanza kazi zetu hapa nchini, tunapenda kuwaaminisha wadau wetu wote kwamba, kampuni hii kwa wakati wote siyo tu kwamba itabakia kuwa mwekezaji, bali pia mdau wa maendeleo ya nchi; tunajiweka kabisa katika mustakabali wa nchi hii kuwa nchi ya viwanda, na serikali inataka ifikapo mwaka 2025, sekta ya madini iwe inachangia zaidi ya asilimia 10 ya pato la taifa, GGM tunataka tuwe sehemu kubwa ya huu mchango,” alisema Shayo.

Akaongeza: “Tunapenda GGM tuwe sababu ya kuchagiza viwanda hivyo au kuchagiza biashara zitakazotumia bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo,” alisema.

Alisema katika kipindi kingine cha miaka 20 ijayo, GGM inataka iwe kama mwekezaji raia na mdau muhimu anayeendelea kuishi na kuambatana na Watanzania katika maendeleo huku ikizingatia umuhimu wa wadau wake ikiwemo serikali na jamii zinazowazunguka.

GGM ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa maonesho hayo yanayofanyika mkoani Geita kwa Sh milioni 200.

Alisema sehemu ya fedha hizo zilitumika kuanzisha mradi wa kituo cha uwekezaji wa biashara katika eneo lenye ukubwa wa ekari 100 zilizotengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita na kutoa Sh milioni 800 kwa ajili ya kuandaa eneo la maonesho ambalo ni sehemu ya ekari 100.

Kwa mujibu wa Shayo, GGM ina teknolojia ya kisasa kuwasaidia wachimbaji wadogo ikiwemo suala la uokoaji na usafishaji wa dhahabu.

Chanzo: habarileo.co.tz