Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GCLA yatakiwa kusimamia usalama wachimbaji wadogo

Mud Matope Madini GCLA yatakiwa kusimamia usalama wachimbaji wadogo

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, amewataka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kusimamia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwafuata na kutoa elimu migoni. Ndemanga amesema hayo jana Agust 25, 2023 mjini hapa, kwenye maonesho ya madini na uwekezaji, huku akisema GCLA ina wajibu wa kusimamia wachimbaji wadogo katika kuimarisha uchimbaji na usalama wa wachimbaji. “Nendeni kwenye migodi...wahini mapema kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo, pamoja na kutoa elimu kwenye migodi na pia mtasaidia kuimarisha uchimbaji na hivyo kuwa endelevu, lakini pia kuhakikisha wakati wote, usalama wa wachimbaji unazingatiwa,” amesema DC huyo. Aidha, Meneja GCLA Kanda Mtwara, Hadija Mwema, amesema kuwa wataendelea kuwakagua lakini pia kutoa elimu juu ya matumizi bora ya kemikali salama. "Tumelipokea tutalifanyia kazi kwa kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji, kuwasajili na kuwakagua ili kuweza kutumia kemikali salama kwaajili ya afya yao,” amesema Hadija. Hata hivyo Mkurugenzi wa GCLA kanda hiyo, Daniel Mndio, amesema kuwa lengo walilokuwa nalo ni kushirikiana, na Tume ya Madini kwa kusajili mwalo yote, ambayo inatumika katika uchenjuaji wa madini, kwa kutumia Zebaki na kujua matumizi yake kama yanatumika kwa usahii. "Lengo, ni kushirikiana na Tume ya Madini kwa kuthibiti mwalo yote, ambayo itatumika katika uchenjuaji wa madini kwa kutumia Zebaki"Amesema Ndalo. Mchimbaji mdogo wa madini ya Namungo, Fadhili Kandala amesema, GCLA ikiwatembelea kwa kutoa elimu ,itakuwa imewasaidia sana kwakuwa wachimbaji wadogo wamekuwa hawajui usalama wao . "Hawa GCLA wakija migodini kutupa elimu, kwakweli watakuwa wamefanya jambo jema, maana sisi kama wachimbaji hatujui kabisa usalama wetu, kwakuwa baadhi yetu sisi elimu haijatufikia," amesema Fadhili

Chanzo: Mwananchi