Jumla ya futi za ujazo Milioni 245 za gesi asilia zinazalishwa kila siku kupitia kitalu cha Songosongo kilichopo wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na kitalu cha Mnazi Bay kilichopo wilaya ya Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame amesema, kitalu cha Mnazi Bay pekee kinazalisha futi za ujazo Milioni 120 za gesi asilia kwa siku.
Makame amesema hayo alipotembelea visima vya gesi asilia eneo la Mnazi Bay mkoani Mtwara, kwa lengo la kuangalia hali ya uzalishaji wa gesi asilia katika visima hivyo na kusema uzalishaji wa gesi hiyo unaendelea vizuri.