Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fursa za kiuchumi zamulikwa Zanzibar

Mfenesini Makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo akiwa na wanachama wa ACT

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman amesema Zanzibar inazo fursa nyingi za kiuchumi na kimaendeleo kwa wananchi wote iwapo kutakuwepo uwajibikaji bora, uadilifu na uaminifu kwa viongozi na wasimamizi wa ngazi mbali mbali.

Mhe. Othman ameyasema Mfenesini wilaya Magharib ‘A’ Unguja alipozungumza na viongozi wa Chama hicho katika mwendelezo wa ziara yake ya Kichama ya kujitambulisha kwa wanachama mbali mbali wa chama hicho tokea alipochaguliwa kushika nafasi hiyo.

Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amesema kwamba mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa rasilimali muhimu zilizopo zinazohitaji usimamizi bora kwa viongozi ili zitumike kuwasiadia wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

Amefahamisha kwamba iwapo kutakuwepo na suala la audilifu na uaminifu na viongozi kusimamia majukumu yao ipasavyo rasilimali na fursa zilizopo upo uwezekano wa kila mwananchi kuwa na ajira na kipato bora na akaweza kuishi maisha ya furaha.

Amesema kwamba kinachohitajika katika kuendeleza rasilimali hizo na ziwe na faida kubwa kwa wananchi wa Zanzibar kwa jumla ni kuwepo ujasiri wa viongozi katika kusimamia kwa uadilifu na uaminifu ili zia wananchi wa sasa na vizazi vya baadae.

Amefahamisha kwamba Zanzibar inazorasilimali nyingi kuliko nchi ya Singapore ambayo pia ni nchi ndogo, lakini kutokana uwajibikaiji na usimamizi bora wa viongozi, hivi sasa nchi hiyo imekuwa ni miongoni mwa nchi tajiri sasa duniani jambo ambalo linawezekana pia kwa Zanzibar.

Akizungumzia suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mhe. Othman, amesema kwamba Tanzania haina kero za muungano kama inavyoelezwa na badala yake kilichopo ni kasoro kubwa za muungano huo ambazo zinazohitaji kurekebishwa ili kila upande unufaike vyema na Muungano huo uliopo.

Amesema ni kosa kubwa kwa baadhi ya viongozi kuacha na kusahau kutetea na kusimamia maslahi ya nchini na badala yake wakasimamia maslahi binafsi jambo ambalo litachangia nchi kukosa maendeleo ya haraka na kuathiri sana mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Akizungumzia suala la ujenzi wa chama, amewataka viongozi kuwajibika vyema katika majukumu yao ikiwa ni pamoja na kukosoana katika njia za kistaarabu ambazo zitasaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho Ismail Jussa, amewataka vijana nchini kutovunjika moyo na kutokata tamaa na badala yake wajitahidi katika kuendeleza chama chao ili kutimiza maelengo ya chama hicho ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kimaendeleo hapa Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live