Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Forodhani sasa mikononi mwa NMB

Images (9)hh.jpeg Forodhani sasa mikononi mwa NMB

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMS) imefikia makubaliano ya kuikabidhi benki ya NMB kutunza bustani ya Forodhani visiwani hapa ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuunga mkono uhifadhi wa mazingira na ajenda ya uchumi wa bluu.

Mradi huo wa utunzaji wa bustani ya Forodhani unalenga kuboresha mazingira ya kitalii na kuakisi vyema sifa maarufu ya eneo hilo, na utawezesha bustani hiyo kuvutia wageni wengi zaidi kila mwaka huku ukichangia kuchochea sekta ya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar wakati wa kutangaza Mashindano ya Mbio za Boti, Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi, Rashid Simai Msaraka alisema benki hiyo imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo na kusaidia utekelezaji wa mipango ya Setikali.

Alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Dk Hussein Mwinyi imeweka kipaumbele cha kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi na kuzitaka kampuni nyingi kuunga mkono mipango ya maendeleo ya serikali.

"Tumefanya kazi kwa karibu na benki hii katika miaka ya nyuma na nimedhihirisha na kutangaza kuwa tayari tumefikia makubaliano ya kuendeleza na kutunza bustani za Forodhani," Msaraka alisema.

Alibainisha kuwa pamoja na kuboresha mandhari ya eneo hilo, mradi huo utaleta manufaa makubwa na kwamba, kazi hiyo itafanywa na wakandarasi wazawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live