Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fistula ya watoto yamliza Rais Samia

Fistula Pic Data Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amesema amesikitishwa na taarifa ya hospitali ya CCBRT kupokea watoto wenye umri kati ya miaka minne hadi 11 wa ugonjwa fistula.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Juni 5, 2022, kwenye uzinduzi wa jengo la kutolea huduma ya afya ya mama na mtoto katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.

Amesema inasikitisha kuona watoto hao wakiugua ugonjwa huo huku sababu kubwa zikitajwa kuwa ni kutokana na kubakwa.

“Nilikuwa nanong’ona na Brenda hapa (Mkurugenzi Mtendaji wa (CCBRT), inasikitisha wana kesi wanazozipokea, mtoto wa miaka 12,11 analetwa hapa ana tatizo la fistula na hii inatokana na watoto kubakwa, wale wanaotubakia watoto wanazalisha tatizo hilo.

“Lakini pia kuna vitoto vidogo kabisa miaka minne, mitano, sita wanapokelewa hapa wana fistula, kwa hiyo ndugu zangu, wana jamii wa Tanzania tuone tatizo hili la ubakaji ambalo kwa kiasi kikubwa tunalifumbia macho huko kwenye jamii” am,esema Rais Samia na kuongeza

“Hatulisemi, hatulipeleki kwenye vyombo vya sheria, wale wanaokosea, matatizo makubwa wanawasababishia wale watoto wetu wanaowafanyia vibaya,”

Alitumia nafasi hiyo kuitaka jamii kupunguza idadi hiyo ya wanaoishi kwa fistula Tanzania kwa kuepuka yale yanayoepukika ikiwemo ubakaji, ndoa za utotoni na mimba za mapema.

“Kitoto cha miaka 12 kinapata ujauzito, kinakuja hapa hakiwezi chochote, anacheleweshwa huko nyumbani, ameanza kusukuma, mtoto anachana kila kitu na mwisho fistula hiyo hapo, kwa hiyo tujitahidini kuacha hizo mila ambazo zinaleta matatizo haya,” amesema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live