Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Finca kumzawadia Sh10 milioni mwenye wazo bora la biashara

20114 Pic+finka TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ili kuongeza uelewa wa stadi za biashara kwa wajasiriamali wadogo, Benki ya Finca Microfinance imezindua shindano litakalomzawadia mshindi wa wazo bora la biashara Sh10 milioni.  

Mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki hiyo, Nicholaus John amesema shindano hilo litaendeshwa kwa kushirikiana na kituo cha runinga cha TV E na litajulikana kama 'kuza ofisi na Finca.’

"Hii ni hatua ya pili la shindano ambapo washindani  wanane wamechaguliwa na jopo la majaji kushiriki katika kipindi cha TV. Mwishoni, mshindi mmoja ataondoka na zawadi ya Sh10 milioni," amesema Nicholaus.

Nicholaus amebainisha hayo leo, Septemba 30, 2018 na kueleza kuwa washiriki wengine wenye vigezo watakuwa na nafasi ya kupata mkopo kutoka benki hiyo. 

Mkuu wa masoko wa benki hiyo, Emmanel Mongella amesema kampeni hiyo ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu huduma zake zianze kutolewa nchini hata kuwa maarufu.

"Ushirikishwaji kifedha na uvumbuzi wa kidigitali ni msingi wa biashara yetu. Shindano hili ni ahadi nyingine kwa Watanzania kwamba Finca ipo kwa ajili ya kuwapa elimu na kuwawezesha wateja kupata maendeleo endelevu ya biashara zao,” amesema Mongella. 

Finca ni sehemu ya mtandao wa Finca Impact Finance, kundi la taasisi zinazotoa mikopo midogo na taasisi 21 za fedha ambazo zinahudumia jamii na kusaidia wajasiriamali wenye kipato kidogo na wamiliki wa biashara ndogo kuwekeza.

Chanzo: mwananchi.co.tz