Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fidia KIA yaiva, Sh11.5 bilioni kutumika

Pesa Fedhaddd Fidia KIA yaiva, Sh11.5 bilioni kutumika

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moshi. Serikali imatakangaza kufikia hatua nzuri za kumaliza mgogoro baina ya wananchi wa vijiji vitatu vinavyouzunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wilayani Hai huku ikibainisha kutolewa kwa Sh11.5 bilioni kwa ajili ya ulipaji wa fidia.

Miongoni mwa vijiji hivyo, ni Tindigani, Sanya Stesheni na Chemka ambavyo kwa miaka 20 vilikuwa na mgogoro wa umiliki wa ardhi na uwanja huo wa ndege.

Haya yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdini Babu, katika mkutano wa waandishi wa habari, ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo, ukilenga kuonyesha mafanikio ya uongozi wa awamu ya sita.

"Tulikuwa na mgogoro na wananchi wanaozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tumeshazungumza na wananchi na tumeelewana kwa asilimia kubwa, tayari tathmini imeishafanywa,” amesema

"... na baadhi ya wananchi wameishaanza kupokea malipo ya fidia baada ya kukubali kufanyiwa tathmini...Serikali imetoa Sh11.5 bilioni kwa kazi hiyo, tunamshukuru sana Rais wetu kwa kufanya kazi kubwa katika hili na amefanya kazi kubwa," amesema

Pamoja na mambo mengine Babu amesema, Serikali imetoa Sh753.92 bilioni kwa ajili ya mkoa huo ili iweze kutumika katika utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, maji, elimu, ujenzi, barabara pamoja na maeneo mengine.

"Katika sekta ya afya Serikali imetoa Sh92.29 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, huku Sh70.30 bilioni zikitolewa kwaajili ya sekta ya elimu, na kwenye ujenzi zimetolewa Sh118.86 bilioni ambazo zitatumika kwenye ujenzi na matengenezo mbalimbali ya barabara,” amesema na kuongeza;

“Ujenzi na matengenezo hayo ni kwa kiwango cha ama lami au changarawe. Vilevile Serikali imetoa Sh367.95 bilioni kwaajili ya sekta ya maji, huku kwenye utalii zikitolewa Sh4.62 bilioni ambazo zitatumika katika uboreshaji wa miundombinu ya utalii," amesema

Naye, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus amesema lengo la mkutano huo ni kuonyesha jitihada ambazo zimefanywa na Serikali ya awamu ya sita katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetengeneza fursa mbalimbali kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live