Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faru weupe kupelekwa Burigi-Chato

White Rhino Faru weupe kupelekwa Burigi-Chato

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) imeiteuwa hifadhi ya Burigi-Chato kuwa miongoni mwa hifadhi mbili nchini zitakazoendeleza na kukuza Faru weupe ambao ni adimu zaidi nchini.

Kupelekwa kwa Fauri weupe katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 22 zilizopo kutaifanya kuwa miongoni mwa hifadhi zenye sifa ya kuwa na wanyama wakubwa watano.

Kwa mujibu wa Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Jonny Nyamhanga ambae pia ni msimamizi wa hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato amesema uwepo wa Faru katika hifadhi hiyo itakuwa kichocheo cha kuongeza wageni na kwamba watalii watapata fursa ya kumpa jina ambalo atalilipia kwa kipindi fulani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live