Sheria na taratibu za kuagiza magari used(Yaliokwisha kutumika) Japan ni kama ifuatavyo;
• Ukaguzi wa JAAI. Magari yanatakiwa yawe yamefanyiwa ukaguzi na JAAI( Japan Auto Appraisal Institute).
JAAI ni taasisi ya Kijapani maalumu kwa kukagua gari used zote na kutoa vibali kwa ajili ya kusafirishwa nje ya Japan. Kwaio kabla hazijaletwa nchini zinakaguliwa kwanza na hii taasisi kuangalia kama gari ina vigezo vya kusafirishwa.
• Kizuizi cha umri wa gari. Tanzania hakuna kizuizi cha umri wa magari japokuwa gari zilizotumika zenye umri kuanzia mika 8 au zaidi huhesabiwa kodi kuanzia mwaka uliotengenezwa hivyo hulipwa kama additional excise duty.
Excise duty ni kodi inayotozwa nchini na Additional excise duty ni aina ya Excise duty ambayo hutozwa kwa bidhaa zote kulingana na kanuni zilizowekwa na nchi. Duh hapa mtarudi kwenye darasa la kodi mpitiepitie.
Tarehe 1 July 2022 serikali ilitangaza vizuizi vya umri kuwa miaka 8 kutoka miaka 10. Kwaio kodi itahesabiwa kuanzia miaka nane ya matumizi.
Hii sheria ya kodi ya kutoza magari yaliyokwisha kutumika ilianza Tarehe 1 July 2014(Commencement of new fiscal year). Hii sheria hutumika kwa magari ya kawaida (Light car) na magari makubwa (Truck) haitumiki kwenye mashine.
Kwaio kuingiza magari kama trucks, Vans, buses n.k hii sheria inawahusu. Mashine kama vile Bulldozer, Grader, Cargo in transit au mashine zote za kilimo hii sheria haiwahusu.
Non utility vehicle huchajiwa rate ya asilimia 25 na Utility vehicle huchajiwa rate ya asilimia 5.
Kodi za magari used kutoka Japan kuja Tanzania ni kama ifuatavyo.
MAGARI YENYE INJINI CC MPAKA 2000 • Import duty asilimia 25 • VAT(Value Added Tax) asilimia 20 • Cumulatively asilimia 50(Dutible Value)
MAGARI YENYE INJINI 2000CC NA ZAIDI • Import duty asilimia 25 • Excise duty asilimia 10 • VAT asilimia 20 • Cumulatively asilimia 65 (Dutible Value)
NOTE: Tanzania hutoza kodi za excise duty kulingana na CC za gari. Injini yenye CC isiyozidi 1000CC haitozwi excise duty.
Document ambazo hutumika Tanzania kuagiza gari kutoka nje. • Bill of Lading. Ni document ambayo huandaliwa na wahusika mfano #beforward kwa ajili ya mteja wao na inakua na maelezo yote kuhusu aina ya gari na mambo yote yanayohusu gari na sehemu itakayotumwa.
• Export certificate • Profoma invoice • JEVIC, QISJ • Agent authorization Letter kutoka kwa importer. • Import Permit kutoka TBS, TFDA n.k.