Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu kuhusu majengo ya kifahari yanayoelea baharini, bilioni 3.5 jengo moja

Nyumba Bahari 2 Fahamu kuhusu majengo ya kifahari yanayoelea baharini, bilioni 3.5 jengo moja

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya wengi kushangazwa na maneo baadhi ambayo yalitumia teknolojia kusogeza maji ili makazi yajengwe kama baadhi ya sehemu za Dubai, basi Wanasayansi hawajawahi kupoa, sasa waleta nyumba za kifahari zinazoelea baharini.

Nyumba zinazoelea ambazo ni ghali sana kumiliki ikiwa ni moja ya teknolojia bora ya nyumba kati ya nyingi zilizowahi kuundwa, imekua stori kubwa maeneo tofauti haswa kwenye mitandao ya kijamii.



Unaambiwa "Ocean Builders", kampuni ya Panama inayojishughulisha na teknolojia ya ubunifu baharini, imezindua nyumba za kwanza zinazoelea baharini zikiwa na sifa ya urejeshaji wa mazingira kwa kuyatunza na kuyalinda.



Kulingana na ripoti majengo hayo yanagharimu kati ya dola za Marekani 295,000 (takribani shilingi milioni 688 za Tanzania) hadi dola milioni 1.5 (zaidi ya shilingi bilioni 3.5 za Tanzania) kwa sasa yanajengwa maeneo ya Linton Bay Marina, pwani ya kaskazini ya Panama huko Marekani Ya Kati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live