Watumiaji wa mtandao wa Twitter wana nafasi ya kutengeneza pesa kupitia maudhui wanayotengeneza na kuweka katika mtandao huo.
Mtandao wa Twitter umeongeza sehemu ya 'monetization' kama Youtube na Facebook.
Watengeneza maudhui watalipwa kupitia 'Twitter Spaces' ambapo watauza tiketi kwa wasikilizaji na vigezo vyake uwe na umri kuanzia miaka 18, uwe umefanya 'space' angalau 3 ndani ya siku 30 na uwe na followers kuanzia 1000. Na hii itafanya kazi kwa watumiaji wa Marekani katika simu za iOS na Android.
Kwenye 'Super Follows' watengeneza maudhui watalipisha followers wao ili kuona baadhi ya maudhui au kumlipa mtengeneza maudhui kwa kitu alichokifanya. Vigezo vyake uwe na followers angalau 1000, umri kuanzia miaka 18 na uwe na tweet zisizopungua 25 ndani ya siku 30. Hii itapatikana kwa watumiaji wa Marekani tu kwa sasa.