Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FCC yawaonya wanaotumia nembo za watu kuuzia bidhaa zao

FCC Onyooo FCC yawaonya wanaotumia nembo za watu kuuzia bidhaa zao

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Tume ya Ushindani wa Haki (FCC) Kanda ya Ziwa imewaonya wafanyabiashara wanaotumia nembo bunifu za watu wengine ili kujipatia fedha ikisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ni kosa la jinai.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Julai 28, 2023 katika ofisi ya FCC jijini Mwanza, Mkuu wa Kanda ya Ziwa, Frank Mdimi amesema kwa atakayebainika kutumia nembo au alama isiyo yake bila ruhusa ataadhibiwa kifungo kuanzia miaka 14 jela, faini au vyote kwa pamoja.

“Wafanyabiashara wajiadhari kutumia nembo zisizo zakwao na zinatumika na watu wengine, lakini kwakuwa bidhaa zenye nembo hizo zinauza basi wao wameona ni vizuri wakawa wanazitumia kusudi wapate pesa; wanafanya kinyume na sheria na waache mara moja kwa sababu tukija kukubaini adhabu utakayokutana nayo tusilaumiane,”amesema Mdimi

Amesema kwa mwaka 2022/23 FCC Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Geita, Simiyu na Mara imefanya ukaguzi na kukamata bidhaa bandia na hafifu ikiwemo vinywaji vikali, filta za mitambo mikubwa inayotumika kwa ujenzi wa migodini, simu na miswaki.

“Nikweli kwamba kumekuwa na changamoto kwa wananchi wengi kuelewa utofauti uliopo baina ya bidhaa bandia na bidhaa hafifu, bidhaa bandia ni bidhaa ambayo inatengenezwa na kuuzwa kiuhadaifu sokoni kwa kutumia alama au nembo ya mtu mwingine bila ruhusa yake,

“Inaweza kuwa imekidhi vigezo vyote vya ubora lakini tatizo linakuja kuwa ni wizi wa miliki bunifu ya mtu mwingine ambao ni wizi na nijinai. Bidhaa hafifu ni ile ambayo haijakidhi viwango vilivyowekwa ama kitaifa au kimataifa kwa ajili ya matumizi salama ya bidhaa husika, kwa mantiki hiyo, bidhaa hiyo mtu atakapotumia inaweza ikamletea madhara,”amesema

Amesema kwakuwa bidhaa bandia zinatengenezwa mara nyingi nje ya utaratibu rasmi, ni kawaida (siyo lazima) kukuta bidha bandia nyingi kuwa hafifu akidai maeneo mengi yanayokuwa nje ya Dar es Salaam changamoto zinakuwa kubwa kwa sababu wafanyabiashara wengi wanajua watu wa mikoani sio wadadisi kwahiyo bidhaa zinazoweza kupelekwa uenda nyingine zikawa na uwezekano wa kuwa hafifu au bandia.

“Mlaji unapokwenda kununua bidhaa hakiki vizuri bidhaa unayokwenda kuinunua, angalia imetengenezwa nchi gani, angalia maelezo ya bidhaa yanafanana na ile uliyoizoea kama ni kifungashio angalia kina umalidadi unaotakiwa na kama unaona huelewi, kunautofauti ahirisha kununua bidhaa hiyo eneo hilo nenda kanunue sehemu inayoeleweka,”amesema Mdimi

Amesema licha ya tume hiyo kuanza kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari lakini amewataka wazalishaji kutoa elimu kwa wasambazaji wao kuhusiana na aina za bidhaa wanazo uza, zipi ni sahihi na zipi si sahihi ili wawe waangalizi katika soko na pale watakapoona kinyume watoe taarifa.

“Matarajio yetu kwa mwaka ulioanzia Julai, 2023, tuendelee kutoa elimu kwa wadau, kuongeza kaguzi mipakani, kuendesha mazoezi ya ufuatiliaji wa mikataba ya mlaji inayoandaliwa na upande mmoja hususani huduma ndogo za kifedha hivyo FCC inatoa wito kwa watoa huduma hao kuwasilisha mikataba hiyo ili iweze kusajiliwa na kuondolewa vipengele vinavyomkandamiza mlaji na kukwepa uwajibikaji,”amesema

Mkazi wa jijini Mwanza, Benadetha John amesema ufuatiliaji wa bidhaa bandia na hafifu utawafanya watumiaji kuwa salama kwakuwa wafanyabiashara wasio waaminifu wataogopa kufanya uhalifu wa kuziingiza nchini kwa njia za magendo.

Chanzo: Mwananchi