Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FCC: Acheni kununua bidhaa zisizo na ubora

Mkurugenzi Mkuu Wa FCC, William Erio FCC: Acheni kununua bidhaa zisizo na ubora

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea wiki ya kupambana na bidhaa bandia duniani kuanzia Juni 8 mpaka Juni 13, 2023 Tume ya Ushindani nchini (FCC), imewataka wananchi kuacha kununua bidhaa zisizo na ubora kwani zinasababisha madhara kwao.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, leo Juni 6, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio amesema tume hiyo ipo kisheria kwa ajili ya kusimamia sheria ya kulinda ushindani kibiashara sambamba na kumlinda mlaji, pia sheria ya kulinda alama inayodhibiti uzalishaji na ulishaji wa bidhaa zinazoingia nchini.

"Bidhaa bandia zinaleta ushindani usio na haki na mara nyingi huwa na bei nafuu, na mara nyingi haitolewi risiti na sio tu unaikosesha mapato serikali ila mlaji anapata bidhaa isiyo na ubora," amesema.

Amesema ili kudhibiti uingiaji na utumiaji wa bidhaa bandia, elimu lazima zitolewe kwa walaji, wafanyabiashara na washafirishaji wa bidhaa za ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live