Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FAO yazindua kikosi kazi uvuvi ziwa Tanganyika

Ziwa Tanganyikauvuvi.jpeg FAO yazindua kikosi kazi uvuvi ziwa Tanganyika

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) limezindua kikosi kazi cha kitaifa kitakachoweza kuimarisha mnyororo wa thamani katika uvuvi wa ziwa Tanganyika.

Akizunguma Februari 14, 2022 mjini Kigoma baada ya kuzindua kikosi kazi hicho,ofisa kutoka FAO,  Hashim Muumin amesema kikosi hicho pia kitaweza kusimamia mradi wa FISH4ACP wenye lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa dagaa na mgebuka wa ziwa Tanganyika.

Amesema kikosi hicho kitakuwa na kazi ya kusimamia mradi huo na kushauri katika maeneo ambayo yatajitaji kuboreshwa ili kuhakiki mradi huo unatoa matokeo chanya katika uvuvi wa ziwa Tanganyika.

Amesema moja ya eneo ambalo mradi huo umejikita kuboresha ni ulinzi shirikishi kwa kushirikisha wana jamii moja kwa moja katika rasilimali za uvuvi lengo ni kuhakikisha wanazilinda kwaajili ya vizazi vya sasa na baadae.

"Katika upande wa uchakataji wa mazao hayo wataenda kuboresha mfumo wa kuanika dagaa kwenye vichanja hali inayowasababishia kupoteza mazao mengi na badala yake watawaletea mfumo wa kukausha dagaa kwa kutumia majiko banifu hatua itakayosaidia kuokoa mazao hayo ya uvuvi," amesema Muumin.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Ishmael Kimirei amesema ili kuendelea kuboresha mazao hayo wataendelea kutoa elimu kwa wadau wa uvuvi na kuhakikisha wanaongeza mnyororo wa thamani wa dagaa na mgebuka wa ziwa Tanganyika.

Advertisement Meneja wa baraza la Taifa la uhifadhi wa mazingira (NEMC), kanda ya Magharibi Benjamin Dotto amesema yeye kama mmoja wa kikosi kazi hicho watakakikisha wanazingatia ubora wa mazao ya uvuvi na ubora wa maji ya ziwa Tanganyika kwa matumizi endelevu.

Mradi wa FISH4ACP ni wa kipindi cha miaka mitano ambapo umeanza mwaka 2020 na kuhusisha nchi 12 na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya na wizara ya maendeleo ya mashirikiano ya uchumi ya Ujerumani na kutekelezwa na Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Kimataifa (FAO), wenye lengo la kuongea mnyororo wa thamani wa dagaa na migebuka wa ziwa Tanganyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live