Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FAO yatoa mamilioni kudhibiti viwavijeshi

Mon, 23 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), limetoa msaada wa dola za Marekani 250,000 sawa na Sh milioni 550 kwa ajili ya kuimarisha teknolojia na ufuatiliaji na kuongeza ufahamu wa kudhibiti milipuko ya visumbufu mazao ikiwemo viwavijeshi.

Viwavijeshi hao hujulikana kwa jina la kitaalamu la Fall Armyworm (FAW) au Spodoptera frugiperda.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa FAO Tanzania, Fred Kafeero alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya uelimishaji juu ya aina mpya wa viwavijeshi (FAW), iliyosomwa mjini Morogoro jana.

Ilisomwa kwa niaba yake na Ofisa Anayerasimisha Masuala ya Usalama wa Chakula na Lishe wa shirika hilo, Stella Kimambo. Mafunzo hayo yaliwashirikisha maofisa kilimo kutoka mikoa 15 na wataalamu wa taasisi, zinazojihusisha na sekta ya kilimo na wakulima hasa wa zao la mahindi kutoka mikoa hiyo.

Mwakilishi hiyo wa Fao alisema shirika limeongeza nguvu hizo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania juu kudhibiti milipuko ya visumbufu mazao kikiwemo viwavijeshi hicho cha FAW.

Hata hivyo, alisema Septemba mwaka jana, Fao ilitoa mitego ya pheromone 216 kwa Wizara ya Kilimo ili kutumiwa kwa ufuatiliaji wa viwavijeshi hivyo nchini, ili kuona uzito wa tatizo hilo na kutoa taarifa muhimu kwa kubuni mipango mipya.

Alisema, mlipuko wa viwavi jeshi vya aina hiyo umeripotiwa mikoa mbalimbali nchini ya Rukwa, Kagera, Pwani, Geita, Simiyu, Kilimanjaro, Njombe, Dodoma, Morogoro, Mara, Katavi, Mbeya, Arusha, Mwanza na Songwe.

Kafeero alisema Fao inashirikiana kwa karibu na nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na wadau wengine kutekeleza mipango muhimu ya kukabiliana na mdudu huyo, ikiwemo kuongoza uelewa kuhusu madhara yake kwa Afrika.

Aisema, viwavijeshi hivyo vina uwezo wa kuongezeka, kuenea na kushambulia mazao tofauti. Alisema kupitia makubaliano hayo, Fao ilikabidhi mitego 216 kwa wizara ya kilimo kutumika katika utafiti na kudhibiti viwavi hao.

Chini ya makubaliano hayo, itatoa mitego mingine 300, hivyo kufanya jumla ya mitego 516 itakayotolewa kwa Wizara ya Kilimo.

Chanzo: habarileo.co.tz