Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FAO kukuza kilimo Tanzania

Tanzania Nchi Ya Tatu Kwa Kilimo Cha Parachichi FAO kukuza kilimo Tanzania

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina mipango ya kuifanya Tanzania kuwa Mzalishaji mkubwa wa chakula ndani ya nchi na ziada kuuza nje ifikapo 2030.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana jioni Jumatatu, Oktoba 16, 2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023.

Waziri Mkuu amehutubia mkutano huo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan na kabla ya ufunguzi wa mkutano huo uliowahusisha Wakuu wa nchi na Serikali, Waziri Mkuu alishiriki katika Maadhimisho ya miaka 78 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live