Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FADev kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wanawake

Tina Ed.jpeg FADev kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wanawake

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Meneja Miradi kutoka katika taasisi hiyo, Evance Lubara, amesema hayo leo wakati wakitambulisha mradi wa jinsia kwenye sekta ya madini, na kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu kwenye uchimbaji wa madini, ambao utatekelezwa mkoani humo, kwa kuanza na migodi iliyopo Msalala wilayani Kahama.

Lubara amesema katika mradi wao wa jinsia, wamejipanga kuwawezesha wanawake kuwaunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ambao ni wachimbaji wadogo, na kisha kuwapatia fedha ili wapate mitaji ya kuendesha shughuli hizo za uchimbaji madini, pamoja na vifaa vya uchimbaji bila riba na kuinuka kiuchumi.

"Taasisi yetu ya FADev tumeanza kuwezesha wanawake ambao ni wachimbaji wadogo wa madini, kuwapatia fedha za ruzuku kwa ajili ya mitaji, ambapo tutaanza na kuwezesha kutoa kiasi cha fedha cha shilingi 500,000 hadi milioni moja kupitia kwenye vikundi, na watakao kuwa wakifanya vizuri wataongezewa ruzuku," amesema Lubara.

Kwa upande wake, Katibu mtendaji wa Taasisi hiyo ya FADev, Tina Mwasha, amesema katika mradi huo, watawapatia pia wanawake elimu ya ujasiriamali, wakiwamo na wanaume, ili fedha wanazozipata ziwekwe kwenye miradi mingine ya maendeleo na kukuza uchumi, ikiwa ipo siku madini yataisha au wao kumaliza nguvu za uchimbaji.

Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoani Shinyanga, Tedyson Ngwale, amesisitiza kuwa kwenye uwezeshaji huo wachimbaji wadogo wa madini ambao ni wanawake, wapewe zaidi vifaa vya uchimbaji madini kuliko fedha, ili kuondoa changamoto ya kuliwa kwa fedha hizo za ruzuku.

Pia Katibu wa chama hicho, Gregory Kibusi, amesema taasisi hiyo imefika katika muda muafaka, ambapo wachimbaji wadogo hasa wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi kwa wakikosa haki zao sababu ya masuala ya mifumo kandamizi zikiwamo mila na mfumo dume.

Chanzo: ippmedia.com