Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Exim yasaini barua ya kuinunu benki ya UBL

Exim yasaini barua ya kuinunu benki ya UBL

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya Exim Tanzania leo Jumatano, Machi 6, 2019, imesaini barua ya kuonyesha nia ya kununua rasmi benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100.

Taarifa iliyotolewa leo na benki hiyo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam

Na naibu ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim, Jaffari Matundu, inasema  ununuzi huo  unaohusisha mali na madeni.

Inasema hatua hiyo inazidi kuifanya benki hiyo ambayo kwasasa ni miongoni mwa benki tano kwa ukubwa hapa nchini kuzidi kujitanua zaidi ndani na nje ya nchi.

“Kwetu ni furaha kubwa kuona kwamba familia yetu inazidi kuongezeka  kwa kuwa tayari tunaungana na wanafamilia kutoka benki ya UBTL,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ya Matundu.

Amesema Exim inaamini kuwa wafanyakazi wa benki ya UBTL nao wataongeza nguvu ambayo kwa pamoja wataweza kutoa huduma bora zaidi za kibenki kwa wateja wa UBTL.

Amesema Exim pia inatarajia kukaribisha wateja wa benki ya UBTL katika mtandao mpana wa matawi ya benki ya Exim huku akiongeza kuwa hatua ya ununuzi huo ni upanuzi wa asili na uimarishaji wa uwepo wa benki hiyo katika soko la ndani.

Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na ndio benki ya kwanza hapa nchini kuvuka mipaka na kujiimarisha nje ya nchi ambapo kwasasa imefanikiwa kuwa na matawi yake katika nchi za Uganda, Comoro and Djibouti.

Tangu kuanzishwa kwake benki hiyo imekuwa ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa wadau wake  na kufikia ukuaji wake kwa kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBTL, Gasper Njuu amesema; “wakati tukiwa kwenye mkakati wa mabadiliko ya kibiashara kupitia uwekezaji kwenye huduma za kidigitali.

Amesema walipopokea ombi kutoka benki ya Exim la kutka kununua benki ya UBTL na baada ya kufikiria kwa kina,  pande zote pamoja na wanahisa walikubaliana.

“Tulifanya hivyo hasa kwa kuzingatia  ubora, weledi na sifa za benki ya Exim kwa hapa nchini ambao kimsingi unaleta tija kubwa kwa wadau na wateja wetu,’’ amesema Njuu.

Benki ya UBTL ilianzishwa mwaka 2013, kama benki tanzu inayomilikiwa na  Benki ya United Bank Limited (UBL) ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Pakistan na imetoa huduma za benki za rejareja na za jumla kwa wateja mbalimbali.

Amesema hatua ya ununuzi inahusisha taratibu kadhaa za kisheria zikihusisha  nchi za Tanzania na Pakistan na zinatarajiwa kukamilika katikati ya  mwaka huu.



Chanzo: mwananchi.co.tz