Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yatoa onyo kampuni zinazoficha mafuta

Mafuta Pic Data (2) Ewura yatoa onyo kampuni zinazoficha mafuta

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (EWURA) imetoa onyo kwa kampuni za zinazohodhi mafuta na kuzitaka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sharia kanuni zinazosimamia biashara ya mafuta ya petroli nchini na masharti ya leseni zao za biashara.

Onyo hilo limetolewa na EWURA leo Jumatatu Julai 17,2023 na kueleza kuwa wamepokea taarifa ya uwepo wa baadhi ya kampuni za mafuta kuhodhi mafuta kwa masrahi binafasi.

Aidha tarifa hiyo imeeleza kuwa zipo kampuni za mafuta zinasemekana kupakia mafuta kutoka kwenye maghala pasipo kuyauza na nyingine kukataa kuuza mafuta kwa wamiliki wa vituo wasio kuwa na ubia au mikataba nao.

“Ewura inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa nchi ina mafuta ya kutosha katika maghala ya kuhifadhia mafuta na meli zenye shehena ya mafuta kutoka nje ya nchi zinaendelea kuingia na kushusha mafuta kama kawaida chini ya uratibu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA),” imesema Ewura Katika taarifa yake ya leo Julai 17, 2023.

Ewura imesema inaendelea kufanya ukaguzi wa kina kwenye maghala na vituo vya mafuta na kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaothibitika kukiuka sheria, kanuni na masharti ya leseni zao, ikiwemo kuwanyang'anya leseni kwa mujibu wa Kanuni Namba 6 ya Kanuni Ndogo za Ukokotoaji wa Bei za Mafuta GN. 57 ya mwaka 2022.

Aidha imesema hadi kufikia Julai 14, 2023 mafuta yote yaliyokuwepo nchini yalikuwa lita 169,853,692 za mafuta ya petroli, lita 209,641,670 za dizeli na lita 34,588,002 za mafuta ya ndege ambayo yanatosheleza mahitaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live