Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yatoa mwelekeo wa bei za gesi za magari

Ureapiic Data Ewura yatoa mwelekeo wa bei za gesi za magari

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati bei ya mafuta ikiendelea kupanda kwenye soko la dunia, hatimaye Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imewasilisha pendekezo la ukomo wa bei ya Sh1, 234.38 kwa kilogramu moja ya gesi itakayouzwa vituo vya kujaza gesi kwenye magari (CNG).

Pendekezo hilo lililotolewa jana Julai 29, 2022 katika mkutano wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu ukomo wa bei hiyo itakayotumika katika vituo vinne tofauti; vituo vikuu, vilivyounganisha gesi kutoka kwenye bomba la kusambaza, vilivyopo nje ya bomba hilo na vidogo vya ugavi na vituo vya magari.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, mchakato wa kupanga bei hiyo ulianza mwishoni mwa Juni mwaka huu na inatarajia kukamilisha hatua zote saba za mchakato Septemba mwaka huu kabla ya kutangaza bei halisi itakayokuwa na usawa kwa wateja na wawekezaji waliojianza kujitokeza ili kujenga vituo vya CNG. 

“Tayari wawekezaji watano kati ya 14 waliopewa vibali vya uwekezaji wa CNG wameshakuja Ewura wanataka kuwekeza, lakini hawawezi kuanza hadi bei ipatikane kwanza kwa hiyo tunategemea kupata bei mpya Septemba,”amesema Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Modestus Lumato leo Julai 29, 2022. 

Kwa kuzingatia bei ya Sh3,220 kwa lita moja ya Petroli ya rejareja katika soko la Dar es Salaam, bei iliyopendekezwa na Ewura ya Sh1,234, itaokoa asilimia 62 ya bajeti ya fedha itakayotumiwa na dereva wa gari lenye mfumo wa gesi asilia. Hii inamaanisha kuwa kila Sh100, atatumia Sh40 ya gharama za nishati.

Pamoja na uwepo wa gesi nchini, tangu 2009 bado kumekuwapo na vituo viwili tu vya CNG: Kituo cha Ubungo chini ya Kampuni ya Uzalishaji Gesi ya PanAfrican Energy Tanzania (PAET) na kile cha Tazara chini ya Kampuni ya Enric Gas Technology Tanzania Limited, vinavyotoza Sh1,550 kwa kilogramu.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Ewura (Ewura CCC), Goodluck Mmari alishauri mamlaka hiyo irekebishe upya bei hizo hususani  uhalisia wa gharama kubwa za uzalishaji na uwazi wa ripoti zilizotumika katika marejeo ya kupanga bei.

“Bei hizo zinaweza kuwaogopesha wawekezaji kama hazitarekebishwa, hatua hiyo itasababisha  watanzania waendelee kuumia na gharama za mafuta,” amesema Mmari.

Baadhi ya wadau wameshauri Serikali kutoa ruzuku na kuondoa ushuru wa bidhaa zote zinazohusika kwenye uwekezaji huo ili kupunguza mzigo wa bei, Baadhi wamekubaliana na pendekezo la bei hiyo huku wakishauri wawekezaji kuonyesha utayari wa kuanza kutumia fursa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live