Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yapiga ‘stop’ upandishaji bei ya gesi

10997 GESI+PIC Mitungi ya Gesi

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imesitisha upandishaji wa bei ya gesi ya kupikia (LPG),

Taarifa iliyotolewa leo Agosti 3 na Ewura na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Godfrey Chibulunje imesema bei hizo mpya zimesitishwa.

“Ewura imebaini uwepo wa baadhi ya kampuni za gesi ya kupikia majumbani (LPG) kupandisha bei za gesi kiholela,” imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa mamlaka hiyo ina jukumu la kulinda masilahi ya wateja.

“Hivyo basi, Ewura inaagiza kusitishwa mara moja upandishwaji wowote wa gesi ya kupikia majumbani mpaka pale itakapopokea na kupitia mapendekezo na hoja za uhalali wa kupandishwa kwa bei hizo,” imeeleza.

Pamoja na agizo hilo, Ewura imezitaka kampuni za uuzaji wa gesi ya LPG kuwasilisha maelezo ya uhalali wa ongezeko hilo mara moja kwa ajili ya uhakiki na mamlaka hiyo ithibitishe pasipo shaka juu ya uhalali wa bei hizo.

“Kampuni yoyote itakayoshindwa kutekeleza maagizo haya ya kiudhibiti itachukuliwa hatua za kisheria,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: Mwananchi