Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yaboresha mfumo wake wa LOIS

Ewura (600 X 315) Ewura yaboresha mfumo wake wa LOIS

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imerahisisha utoaji leseni za usanikishaji mifumo ya umeme kwa kuboresha mfumo wake wa LOIS unaotoa huduma za leseni kwa njia ya kieletroni.

Hayo yameelezwa na Mhandisi Mwandamizi wa Umeme kutoka EWURA Nicholaus Kayombo, wakati akitoa elimu kwa Wanafunzi wanaosomea usanikishaji mifumo ya umeme katika chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi -VETA Iringa.

Amewataka Wanafunzi hao kuhakikisha wanapata leseni hizo kutoka EWURA pindi wanapomaliza masomo yao ili kukidhi matakwa ya sheria, usalama na ubora wa huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live