Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ewura yabaini janja usafirishaji mafuta, yaonya wanaohodhi

Wamiliki Wa Magari Kenya Waingia Tanzania Kununua Mafuta Ya Bei Rahisi Ewura yabaini janja usafirishaji mafuta, yaonya wanaohodhi

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (Ewura), imegundua mchezo ‘mchafu’ wa kuhodhi mafuta kwenye maghala, jambo linalosababisha kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo katika mikoa kadhaa nchini.

Mkurugenzi wa Ewura Dk James Andilile amesema kilichopo ni kwamba magari yanayopaswa kusafirisha mafuta, yanatumia muda mrefu yanapofika kwenye maghala hayo na hivyo kusababisha maeneo yenye uhitaji wa mafuta kukosa nishati hiyo katika muda muafaka.

“Unakuta gari linaenda ghala ‘A’ kuchukua mafuta, likifika linaelekezwa kwenda ghala jingine, hivyo muda unapotea,” amesema Dk Andilile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 20, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bosi huyo wa Ewura, nchi ina mafuta ya kutosha na kwamba mamlaka ilikuwa ikijiuliza sababu za baadhi ya maeneo kukosa mafuta, jambo lililowalazimu kufanya ukaguzi katika ‘depo’ kubwa za mafuta kwa lengo la kujua maeneo yenye changamoto.

Dk Andilile amesema baada ya kutembelea ‘depo’ hizo wamegundua upangaji wa magari kuingia na kutoka ghala moja kwenda jingine ndiyo chanzo cha madereva kushindwa kufikisha mafuta kwa wahitaji katika muda muafaka.

Onyo kali latolewa

Aidha Dk Andilile amewaonya wale wote wanaohodhi mafuta kwa kigezo cha kungoja bei ipande amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria

"Yeyote atakayethibitika anafanya mchezo huo, atachukuliwa hatua stahiki za kisheria. Suala la mafuta ni uchumi wa nchi. Hatutaruhusu mtu afanye mchezo na suala hili,” ameonya vikali.

Mbali na kuwaonya wafanyabiashara hao, Dk Andilile amewaonya pia wale wenye tabia ya kuuza na kununua mafuta kwenye vidumu kuwa wanakosea kisheria na endapo wakikamatwa watachukuliwa pia hatua.

Mwisho amewatoa hofu Watanzania kwa kusema mafuta yapo ya kutosha nakwmba mamlaka yake imekubaliana na wasambazaji wa bidhaa hiyo kufanya kazi usiku na mchana ili maeneo yote yafikiwe kwa wakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live